DAYNA NYANGE AFUNGUKA JUU YA WASANII WANAOPENDA KUANDIKIWA NYIMBO - BZONE

DAYNA NYANGE AFUNGUKA JUU YA WASANII WANAOPENDA KUANDIKIWA NYIMBO

Share This
ENTERTAIMENT: Msanii wa bongo fleva Dayna Nyange ambaye kwa sasa anafanya vizuri na chupa aliloliachia kwa kushtukiza akiwa amemshirikisha Billnass “Komela”.
Dayna Nyange amefunguka na kuwasihi wasanii wa kike nchini kujifunza kuandika nyimbo zao wenyewe ili kuweza kupata ‘melodi’ na mizuka ya kuimba nyimbo nzuri.
Dayna adai, “siyo vibaya kuandikiwa wimbo lakini kwa wakati mwingine ni vizuri kujua kujiandikia mwenyewe kwani unaweza kupata zali la kuingia studio kubwa hata nje ya nchi na kupata nafasi ya kurekodi hata na wasanii wakubwa ukashindwa na ukapoteza zali kwa kuwa hujui kuandika”. Alisema kwenye eNewz
Pia Dayna hakusita kumwagia sifa msanii mwenzake Maua Sama kwani anadai aliwahi kusikia kuwa ni mmoja kati ya wasanii wa kike wanaoweza kujiandikia nyimbo na kumsifia kwamba ni mwandishi mzuri.

No comments:

Post a Comment

Pages