Ditto: Sikutarajia kupata heshima niliyoipata kwenye ‘Moyo Sukuma Damu’ - BZONE

Ditto: Sikutarajia kupata heshima niliyoipata kwenye ‘Moyo Sukuma Damu’

Share This
ENTERTAIMENT: Hitmaker wa ‘Moyo Sukuma Damu’ Ditto amefunguka kuwa hakutarajia kuona heshima inayoupata wimbo wake huo hivi sasa.
Ditto ameiambia Bongo5, “Ukifanya kazi unatarajia unafanya kazi nzuri lakini kiwango cha namna watu watu wanapokea sidhani kama yupo mtu anaweza akakadiria ni namna gani watu watapokea ile kazi. Siwezi kusema nilitarajia kama itapokelea hivi lakini nilijua nimefanya kazi nzuri na watu watasipenda.”
“Reaction ya watu wanaponiona kwanza, unajua sisi artist unatoka unaenda kwenye interview kituo fulani kikubwa cha redio ukifika hata ile reaction ya watangazaji wakikuona unaona kabisa ule wimbo umewashika kwa kiasi kikubwa, ukifika mlangoni hata kama ni walinzi watasema njoo tupige picha kwanza .”

No comments:

Post a Comment

Pages