Hizi ndio Ngoma Kali za Wiki Zilizofanya poa Toka majuu na Bongo Ukianzia na Kanye West, Pusha-T na Wengine wengi..! - BZONE

Hizi ndio Ngoma Kali za Wiki Zilizofanya poa Toka majuu na Bongo Ukianzia na Kanye West, Pusha-T na Wengine wengi..!

Share This
Karibu Juni..!! Ni kipindi cha Baridi hiki pamoja na kati ya mwaka kwenye kihistoria hii ndio wiki tamu sana kwa mashabiki wa Mziki Mzuri. 

Image result for top songs

Vitu Vingi sana Vimebadilika na zaidi kwa magwiji wanavozidi kujitunza kwa majuu tunaona wanatoa Album kubwa sana zinadondoka tuu kibongo bongo kuna kitu tunatakiwa kujifunza kuna Soundtrack za Jams pale unapokuwa unaenda kwenye maeneo ya Beach na usiku unapokuwa umetoka na marafiki pamoja na zile ngoma ambazo upo mwenyewe umetulia.
Bzone tumekuwekea ngoma ambazo zimekimbiza wiki hii kutokea majuu na hata baadhi zikikimbiza Bongo.

Image result for kanye west yikes

Kama ulimsikia Kanye West na ishu yake ya Album ya Ye ikiwa bado haijatoka kwa masiku ambayo ilikuwa inatarajiwa kutoka huku baadhi ya ngoma zikipata wasaa wa kuskilizwa kwa masaa 11 kabla haijatoka Full Album nzima ikiwemo Ngoma ya "Yikes" ikisikilizwa sana na wadau ngoma hii imekuwa pendwa sana kwasababu Kanye anarap kupitia Trap Drums Patterns na kujiongelea yeye mwenyewe hakika inakufanya huwe makini sana kuisikiliza.

Image result for diamond platnumz iyena

Kibongo Bongo kama umepata wasaa wa kuisjikiliza hii kutoka WCB ngoma ikitokea kwenye Album ya A Boy From Tandale ya Diamond Platnumz akishirikiana na moja ya msanii wake kutoka kwenye Record Label iyo ngoma inajulikana kama "IYENA" niamini ni ngoma moja hivi yenye mahadhi ya Kiafrika Mashariki imeleta usikilizwaji mzuri sana kwenye masikio ya watu wengi.

Related image

Tukiwa tuangelea G.O.O.D music ndio hivi kama ujapata kumsikiliza Pusha-T nazani utakua umefanya makosa makubwa sana mtu wangu ebu achana na ile ya kusema kwasasa hana bifu lolote na Drake ebu jaribu kuisikiliza ile "Duppy Freestyle" aliofanya kwajili ya Drake.

Image result for pusha t duppy freestyle

Na hii nyingine ya Pusha-T akiwa ameshirikiana na Future ikiwa ni ngoma ambayo itakuja kusikika kwenye Moja ya Filamu ambazo bado haijatoka ngoma ikijulikana kama BAG.

Related image

Nyingine ni kutoka kwa ndugu zangu ROSTAM wakishirikiana na Khaligraph Jones ngoma ikijulikana kama 'Now you Know' kwenye hii ngoma namuona Stamina mwengine kabisaaa kwasababu jinsi alivyoweza kuflow na ufundi alioutumia kwenye ngoma hii ukumchukua pamoja na Khaligraph ambae amekaa kwenye kiitikio.

Image result for lil mama

Hebu turudi moja kwa moja Amerika kwenye pande wa Kusini yani mpaka kwenye jiji la New York mji wa Rap tukiwa tunamgeukia Lil Mama mbae ameweza kuwika na "Shoe Game" ikiwa ni dance song ikiwa imefanyiwa mix ya kutokea beats za mwaka 2000 huku A$AP Ferg akitoa ngoma mpya lakini imekuwa pendwa vibaya mno kila kona nayokatiza nakutana nayo "Harlem Anthem" hii ngoma imekuwa ikisikilizwa mara kwa mara kwasababu humu tunamsikia A$AP mwengine kabisa sio yule tuliomzoea.

Ungana na mimi Wiki Ijayo tuweze kujua ni ngoma gani zimefanya poa ndani ya wiki..!

No comments:

Post a Comment

Pages