Barnaba Kuachia Album Mwezi ujao..! - BZONE

Barnaba Kuachia Album Mwezi ujao..!

Share This
Barnaba ameweka wazi kuwa amekamilisha albamu yake ambayo inatarajiwa kutoka mwezi ujao Albamu ya muimbaji huyo ambayo inakwenda kwa jina la Gold itakuwa na nyimbo zipatazo 18. Kupitia ukurasa wake wa Instagram ndipo ameeleza kukamilika kwa albamu hiyo.

Related image

Awali albamu hiyo ilipangwa kutoka February 2018 lakini ikahairishwa hadi July 2018 kutokana na kile Barnaba alichoeleza kuwa wadhamini wake wakuu watatu walipendelea hivyo.
Mwanzoni mwa mwaka huu katika kipindi cha The Playlist, Times Fm, Barnaba alisema albamu hiyo itakutanisha wasanii wengine kutoka Kenya Uganda na Nigeria.
Related image
Wasanii waliotajwa kuwepo katika albamu hiyo ni pamoja na Juliana Kanyomozi na Jose Chameleon kutoka Uganda. Kutoka Bongo kuna Vanessa Mdee, G Nako, Ben Pol, Aslay, Barakah The Prince, Linex na Joh Makini.
Image result for Barnaba

No comments:

Post a Comment

Pages