
Na sasa wamelizia kumuingiza kocha msaidizi wa Manchester United Faria ambae ni msaidizi wa mda mrefu wa kocha Jose Mourinho na Arsenal wameonesha nia yao kwa kocha huyo.

Faria mwenye umri wa miaka 42 amefanya kazi na Mourinho tokea mwaka 2001 mara ya kwanza akiwa kocha wa viungo na baadae kuwa kocha msaidizi.
Lakini inaaminika kuwa Mreno huyu anao uwezo wa kuwa kocha mkuu na kama Arsenal watakua na nia ya kweli kwa kocha huyu, mmiliki wa washika mitutu Stan Kroenke ambae amewaajili makocha kadhaaa kwenye sekta za michezo nchini Marekani.
Arsenal wanaelewa hali halisi inavyokuwaga pale unapoachanan nakocha aliekaa kwa mda mrefun kwenye klabu kwahiyo wanajitahidi kuweka mipango mizuri ya kumpata mrithi sahihi wa Arsenal na namba moja ikiwa inakamatwa na kocha wa Juventus Max Allegri.
No comments:
Post a Comment