“Imagine mtu unalipa kodi halafu kazi yako au bidhaa yako hailindwi? Utawezaje kulipa kodi hiyo huko mbeleni? " FIDQ - BZONE

“Imagine mtu unalipa kodi halafu kazi yako au bidhaa yako hailindwi? Utawezaje kulipa kodi hiyo huko mbeleni? " FIDQ

Share This
Baada ya  siku moja toka rapa, Fid Q ateuliwe na Chama Cha Muziki wa Kizazi Kipya nchini (TUMA) kuwa Mwenyekiti wa kamati ya Fedha, Mipango na Uchumi, amenza kazi kwa kuwasilisha ombi la kutaka kutambuliwa na kuundiwa sera yake kwa sanaa ya muziki Bongo ili uweze kujitegemea.




Fid Q ametumia siku ya Wafanyakazi kutoa ombi hilo kwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, ikiwa ni siku moja tu tangu ateuliwe na Chama cha Muziki wa Kizazi Kipya Tanzania (TUMA), kuwa Mwenyekiti wa kamati ya Fedha, Mipango na Uchumi.

“Sanaa ni sekta rasmi hivi sasa lakini bado haijapewa sera na hiyo ni sawa na kuwa na ofisi isiyokua na KANUNI, TARATIBU wala SHERIA. Kwa ufupi bado tunaongozwa na sera ya utamaduni. Tunayofuraha kubwa ya kuitumia sikukuu hii ya wafanyakazi kwa kuikumbusha WIZARA na SERIKALI kwa ujumla kutuundia sera ili SANAA yetu iweze kuleta tija kwenye jamii. (Na katika hilo tunashauri RASIMU iandaliwe na WASANII wenyewe). ameandika Instagram..
Aidha Fid Q ameongeza kwa kusema wasanii wanalipa kodi kwa kazi zao za sanaa lakini kazi zao hazilindwi na serikali, kitu ambacho kinatishia usalama wa wao kuendelea kulipa kodi siku za usoni kwani hawatakuwa wanatengeneza faida.

“Imagine mtu unalipa kodo halafu kazi yako au bidhaa yako hailindwi? Utawezaje kulipa kodi hiyo huko mbeleni? #Meimosi njema waungwana – FK ( Mwenyekiti Wa Kamati ya Fedha, Mipango na Uchumi TUMA ),” aliongeza Fid Q.

No comments:

Post a Comment

Pages