

Waitaliano walichukua dakika sita tu kuongoza kupitia Edin Dzeko kwa kuwapita Jirdi Alba na Samuel Umtiti baada ya kupokea through ball iliotokea kwa De Ross na kumvesha pia kipa Andre Ter Stegen.
![]() |
Dzeko alipowapa Roma goli la kuongoza |
Roma walilazimisha goli la pili na Ter Stegen baada ya kuupangua mpira uliopigwa kichwa na Edin Dzeko na kuwa kona pamoja na shuti lilopigwa na kugonga nguzo.
Walistahili kupata goli la pili kwenye dakika ya 58 pale Dzeko alipobanwa asiweze kupita kwenye eneo la kufunga na aliangushwa na beki mkongwe Gerad Pique.
![]() |
kulikuwa na goli la Pili kutoka kwa De Rossi |
Daniele De Rossi aliweza kupata nafasi ya kupiga mwaju wa penati na kuwafanya Roma kuitaji goli moja tuu la ziada ili waweze kusonga hatua inayofuata ambalo lilitokea kwenye dakika ya 82 kupitis kichwa cha Kostas Manolas.
Wakatalunya walikuja Roma kwa kujiamini kwamba watasonga hatua nyingine tena baada ya kuwa wanaongoza ligi kwa alama 11 zaidi ya wababe wawili kutoka Madrid na kuingia kwenye fainali za Copa del Rey.
![]() |
Messi akiwa kwenye uzuni baada ya mabo kwenda ndivyo sivyo kwa Barcelona. |
Messi alipata nafasi kadhaa ya kupiga mipira iliokufa lakini mambo yakawa bado tofauti kabisa mipira ikiwa inapita juu ya goli. Tulitarajia kwamba Ernest Valverde anaweza akawashika masikio wachezaji wake ili waweze kujipatia goli la ugenini moja tu.

Ni msimu mwengine tunamaliza na kuwaona Barcelona wakiwa na ladha ya uchachu kwenye mdomo wao huku wapinzani wao Real Madrid wakiwa wanaliwinda kombe ilo kwa mara ya tatu ,mfululizo.
![]() |
Jesus alikuwa na bahati sana ya kutolewa kwenye mchezo. |
Kombe la mabingwa Ulaya ndio kombe linalo wanyima raha sana kwa miaka ya hivi karibuni kwasasa huku wakiwa wanajiandaa kutangaza ubingwa wa ligi kwa wiki kadhaa zijazo na kulibeba lile la Copa Del Rey kama wakiwapiga Sevilla kwenye fainali.
Mbali na hiyo watakuwa wanaitazama fainali ya Kombe la klabu bingwa Ulaya wakiwa na wivu wa kupindukia kwenye sofa na itakua mbaya zaidi kama Real Madrid wakilibeba kwa mara nyingine tena.

No comments:
Post a Comment