CHEKI JINSI JAVIER HERNANDEZ ALIVOZIPANGUA ZILE ALAMA MBILI KWA CHELSEA ..OFU YA KWENDA EUROPA YATANDA KWA CONTE. - BZONE

CHEKI JINSI JAVIER HERNANDEZ ALIVOZIPANGUA ZILE ALAMA MBILI KWA CHELSEA ..OFU YA KWENDA EUROPA YATANDA KWA CONTE.

Share This
Javier Hernandez alizipangua alama kadhaa kwa Chelsea na kuipa nguvu timu yake ya kuzidi kujitoa kwenye mawazo ya kuweza kushuka daraja na kuwapa msongo wa mawazo Chelsea.

Wachezaji wa Chelsea wakishangilia goli la Azpilicueta

Cesar Azpilicueta mapema tu aliwapeleka kifua mbele wanadarajani lakini mbali na hiyo walitawala kila idara huku wagonga nyundo wakijitahidi kuimili mikiki ya Chelsea kwa kufanya baadhi ya uwokozi iliobora.

Noble na Hernandez wakishangalia goli la kusawazisha

Na pale Gary Cahill alipoweza kuzuia kichwa kilicho miminwa na Marko Arnautovic  na mpira kurudi tena ndani ya chumba na kukutana na mviziaji mwenye asili ya kimexican na kuunganisha mpira huo moja kwa moja wavuni na kufanya matokeo yawe sare ya 1-1

Willian alipo pokea mpira na kukutana na Joe Hart

Goli pekee la Chicharito kwa West Ham

David Moyes  kwa upande wake alama ata moja ilikuwa na thamani kubwa sana kwake yeye na kumfanya kuzidi kuikimbia safari ya kushuka daraja, Ebu ngoja tumkumbushe Conte  kwasasa anaalama 57 alama 3 zaidi ya Arsenal ambaye yupo nafasi ya sita shauri yake na yeye Uefa ataiota.

No comments:

Post a Comment

Pages