NI KWELI SERGEJ MILINKOVIC SAVIC NDIO JIBU LA KIUNGO CHA MANCHESTER UNITED? EBU KUTANA NA KIUNGO WA LAZIO ANAETOKEA TAIFA LA SERBIA. - BZONE

NI KWELI SERGEJ MILINKOVIC SAVIC NDIO JIBU LA KIUNGO CHA MANCHESTER UNITED? EBU KUTANA NA KIUNGO WA LAZIO ANAETOKEA TAIFA LA SERBIA.

Share This


Ni rahisi sana wachezaji wadogo kujitangaza wao wenyewe kwenye Dunia miaka hii ya karibuni.



Youtube na sehemu za mitandao ya kijamii kila kitu kipo humo.

Mbali na hiyo Historia ya Sergej Milinkovic savic ambae amekuwa na msimu mzuri akiwa na klabu kutokea Italia, Lazio.

Milinkovic -Savic anafurahia sana msimu wake ndani ya Lazio kila mtu analijua hiloo ata Manchester United.

Akiwa kama anatazamiwa kama kitu  kikubwa kwenye Serie A mchezaji huyu mwenye umri wa miaka 23 ameweza kutumikia taifa lake la Serbia kwenye timu yake ya Taifa mwaka wa jana na anategemewa  kuwa kianzio cha Mladen Krstajic kwa miaka inayo kuja.



United wanataarifiwa kuanza kufanya mazungumzo rasmi pale msimu utakapo isha tuu  huku Liverpool na Manchester City inasemekana nao pia wanamnyemelea kiungo huyo.

Mbali na hiyoo wa Italiano wengi hawakutarajia kuona kiwango hiki cha Milinkovic alichokifanya akiwa na Lazio kocha Simone Inzaghi anataka aendelee kumshikilia kwajili ya msimu ujao..



Ila mda ndio utasema kila kitu, ndio kwa mda gani lazio watamshikilia lulu hii na nje kuna timu kibao zenye ushawishi?

 

Miliknovic-Savic anaweza akaonekana akiwa kama uboreshaji mkubwa kwenye kikosi cha United baada ya kuondoka Maroune Fellain ambae mkataba wake unaisha msimu huu.

Kama akitua ndani ya United anaweza akaleta usaidizi mkubwa kwa Jose Mourinho ambae ana mipango ya kutumia viungo watatu hakiwajumuisha Nemanja Matic na Paul Pogba.



Je unajua kama Savic anadamu ya kimichezo kabisa?



Familia yake ni wanamichezo wote huku baba yake akiwa mchezaji wa zamani kwenye mpira wa miguu huku mama yake akiwa mchezaji wa zamani kwenye mpira wa kikapu, Kaka yake ambae anajulikana kama Vanja ambae anadakia Torino na ambae alikuwa amebakia kidogo kutua United mwaka 2015.

No comments:

Post a Comment

Pages