SIENDI POPOTE MIMI..!!! ARSENE WENGER AMEENDELEA KUSISITIZA KWAMBA HANA MIPANGP YOYOTE YA KUONDOKA ARSENAL. - BZONE

SIENDI POPOTE MIMI..!!! ARSENE WENGER AMEENDELEA KUSISITIZA KWAMBA HANA MIPANGP YOYOTE YA KUONDOKA ARSENAL.

Share This
Arsene Wenger ameendelea kusisitiza hana mipangp yoyote ya kuondoka kwenye klabu hiyo ya Arsenal msimu huu na ataendelea mpaka mwaka 2019

Wenger maisha yake ya kwenye klabu yameanza kutiwa dosari baada ya kutajwa kwa mtu ambae atakuja kumrithi pamoja na Carlo Anceloti kutajwa zaidi akiwa kama mtu atakae kuja kumrithi pale Arsenal na kwasasa tunaweza kuona klabu inapitia changa moto kubwa ya kuweza kuwa kosa wachezaji wake muhimu kama vile Mesut Ozil na Alexis Sanchez ambao wamebakiza miezi sita tuu kwenye mikataba yao..!

Kocha wa washika mitutu huyo ameweza kukubali kwamba Alexis Sanchez atauzwa mwezi huu kwasababu amekataaa kuongeza mda wa mkataba wake  lakini akasema hana nafasi kubwa sana ya kuweza kumshawishi Mesut Ozil ili kuweza kubaki na kuongeza mda wa mkataba wake na hakiwa hanatarajia wino wa Jack wilshere kuongeza mda.

Wenger. 68, ameendelea kukaza uzi na kamba kwa kubana kabisa na pini juu ya uwepon wake ndani ya dimba la Emirates na hataki kurudia kile kilichotokea msimu uliopita kutoshiriki klabu bingwa ulaya.

Lakini hatimaye Wenger amesema kutokea kwenye uvungu wake wa moyo na kusema kwamba haendi popote..!! "siku zote nina nia. Niko hapa takribani miaka 21." Alisema Wenger.

"kwahiyo kwenye kila maamuzi nayofanya nafanya kile kilicho sahihi kwenye klabu. Kama nikikaa kwa mwaka mmoja au kumi ni bora zaidi ile ya nyuma.
"ni mimi naendesha au mtu mwengine ambae anafanya kile kilicho bora kwa klabu. Na iko ndio tunacho jaribu kukifanya na haviingiliani kabisa na mambo binafsi."

No comments:

Post a Comment

Pages