MALCOM NI NANI? - BZONE

MALCOM NI NANI?

Share This
Arsene Wenger yupo kwenye foleni ya kulipa pauni miliono 45 kwajili ya kumdaka mshambuliaji wa kibrazili ambaea anaweza akawa mzibaji pengo halisi wa Alexis Sanchez.

Sanchez anatakiwa na Manchester City na vile vile mawasiliano yameshafunguliwa juu ya uhamisho wake mwezi huu, Arsenal wanafanya kila liwezekanalo kupata mtu wa kuziba nafasi yake, na ndio kinacho wafanya washika mitutu kuanza kumfukuzia Malcom 20 ambae ameweza kuwika msimu huu.

winga huyo ambae ametumikia miaka miwili na klabu ya kifaransa na anafaa  kukaa nafasi ya Sanchez.

Hapa nimekuwekea kila kitu unachotakiwa kukijua kuhusu yeye..!!

JINA KAMILI: Malcom Filipe Silva de Oliveira, anajulikana kama Malcom

SEHEMU YA KUZALIWA: Sao Paulo,Brazili

NAFASI: Mshambuliaji

TAREHE YA KUZALIWA: 26 Februari 1997

KLABU ANAYOCHEZEA: Bordeaux

JEZI NA: 7Malcom

HISTORIA YAKE

Ameanza historia yake ya kucheza soka kwenye ardhi ya nyumbani  akiwa na Corinthias, Malcom akafanya uhamisho wa kwenda Ulaya mwaka 2016 akienda kwenye klabu ya kifaransa.

Winga huyo wa kushoto ambae alijiunga na ligi ya ufaransa akiwa na klabu ya Bordeaux kipindi cha usajili mdogo Januari akiwa na umri wa miaka 18.
ameshaweza kucheza michezo 73 na kushinda magoli 10 kwenye klabu yake.
kwa kuongezea kabla ya kuingia Ufaransa alishaweza kucheza michezo 13 kwenye kikosi cha Brazili chini ya umri wa miaka 20 na akishinda mara 2 na akaweza kucheza kombe la dunia chini ya miaka 20 mwaka 2015 Serbia.Malcom

Baada ya kutua Bordeaux maisha yake mapya yaliweza kumfanya aweze kuanza michezo mitano tuu tangia aanze miezi yake mitano ya ufunguzi  na klabu (michezo 13,magoli 2)

Malcom aliweza kujifanya haraharaka kuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi icho katika dimba la Matmut Atlantique msimu uliopita akiwa winga wa upande wa kushoto chini ya kocha Jocelyn Gourvennec.

Huku Bordeaux ikiweza kumaliza nafasi ya sita kwenye ligi na kupata nafasi ya kuweza kushiriki Europa Malcom aliweza kucheza michezo 45 kwenye michuano yote akishinda mara 9 na akitoa assits saba.

Mbali na msimu huu ameweza kucheza mara 21 na akitumia dakika 1,724 na akifanikiwa  kumaliza dakika 90 kwenye michezo 14

JE UNAZANI MALCOM NI CHAGUO SAHIHI KWA ARSENAL?
https://www.polleverywhere.com/multiple_choice_polls/hMaszCg5f5184fx/embed#No comments:

Post a Comment

Pages