Ukiwa unafikilia wachezaji tajiri zaidi duniani kwa haraka haraka unaweza ukafikilia kama Cristiano Ronaldo, Lionel Messi na Neymar sio kwa kijana mwenye umei wa miaka 19 ambae anaichezea klabu ya Leceister City.
Kutana na Faiq Bolkiah mpwa wa Sultan kutokea Brunei (Hassanal Bolkiah) ambae hana thamani ya zaidi $20 milioni.
Winga huyo wa mbwa mwitu mwenye kipaji cha haina yake amecheza Uingereza kwa mda mpaka sasa akianza career yake ya soka kwenye timu ya AFC Newbury kama mtoto mdogo hivi.
2009 Southampton walimchukua Bolkiah kwenye academy yao mbali na kutopewa mkataba lakini Arsenal walimpa Ofa ya mkataba mwaka 2013
Bolkiah alishandana na Washika mitutu kwenye kombe la Lion city cup 2013 na akatupia magoli kwenye mashindano hayo.
Mbali kuwa na hali yake hiyo, Chelsea nao wakatoa ofa yao kwa winga huyo ikiwa ni dili la miaka miwili ambalo akafanikiwa kuweka sahihi yake lakini baada ya mwaka mmoja Bolkiah alienda kulichezea taifa la Brunei na kuliwakilishabtaifa lake mara tisa na akishinda mara moja.
Ili nikupe wazo la utajiri wa Bolkiah lazma kwanza unatakiwa umuangalie baba yake kwanza, Jefri.
Sultan wa Brunei ambae ni kaka yake aliweza kuweka miradi yenye thamani ya £10bn ndani ya miaka 15 na vile vile Jefri anatumia £35m kwa mwezi kununua magari, saa na peni zenye dhahabu.
Iliaminika baba wa winga huyo hanamiliki zaidi ya magari 2300 yakiwemo Bentleys, Ferrari na Rolls Royce.
Amejenga uwanja mzima kwa jili ya party yake ya siku ya kuzaliwa na aliweza kumleta Michael Jackson akimlipa £12.5 m
Kwa utajiri wote watu wanajiuliza ndio acheze mpira jamani kwanini anajisumbua kucheza soka. Lakini Bolkiah binafsi wakati hanaojiwa akasema “nimecheza mpira tangia nikiwa mdogo na nina weza kukumbuka nikiwa na umri mdogo sana nilikuwa niki enjoy nikienda nje ya uwanja nikiwa na mpira mguuni kwangu. Wazazi wangu siku zote wamekuwa kwanipa sapoti ili kuweza kufikia ndoto zangu za kuwa mchezaji. Walinipa mazoezi yote ya kiakili na kimwili kipindi cha utoto wangu, kwahiyo naweza kusema ni kati ya watu mashuri kwangu mimi.”
Home
Unlabelled
KUTANA NA MCHEZAJI TAJIRI ZAIDI DUNIANI; FAIQ BOLKIAH ANAIEICHEZEA LECEISTER CITY NA NI MPWA WA SULTAN KUTOKEA BRUNEI
KUTANA NA MCHEZAJI TAJIRI ZAIDI DUNIANI; FAIQ BOLKIAH ANAIEICHEZEA LECEISTER CITY NA NI MPWA WA SULTAN KUTOKEA BRUNEI
Share This
Share This
About Bwherever
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Bwherever is a Tanzanian Radio Personality and Blogger who initiative Bbaseonpoint blog.
No comments:
Post a Comment