MSIMU MPYA WA UEFA NA MAMBO MAPYA - BZONE

MSIMU MPYA WA UEFA NA MAMBO MAPYA

Share This
NA ABDUL KHALID,
SPORTS: Kama ni mpenda soka bila shaka kipindi hiki utakuwa karibu zaidi na runinga yako kuifatilia timu yako katika mashindano makubwa zaidi ya klabu bingwa ulaya maarufu kama UEFA CHAMPIONS LEAGUE.

Mshindano haya ulaya  yameanza rasmi kutimua vumbi usiku wa jana ambapo tulipata kushuhudia mechi baina ya wababe mbalimbali ambazo tuliona  matukio ya kusisimua, kuvutia huku mengine yakiwa na ubabe ambayo kwa kiasi chake yameweza kutuonjesha walau kidogo ile ya ladha ya mashindano haya pendwa Duniani.

kupitia michezo ya jana tumeweza kuona kwa pamoja  kila timu ikiwa na lengo la kuishangaza dunia kupitia sajili walizozisajili katika msimu huu.

HISTORIA ZA KLABU

Katika mashindano haya kila klabu ina historia yake katika michuano hii na kila timu inahitaji kufanya vizuri ili kuendelea wasifu zao zilizojengwa na magwiji wao, hapa timu nyingi hujipa moyo na mara nyingine huwasaidia  kuwajenga kisaikolojia wachezaji kulingana na mchezo husika japo mara nyingine hugonga mwamba na mwisho tunaishia kusema haikuwa bahati.

TAKWIMU

Katika michezo ya ufunguzi iliyochezwa hapo jana tumeweza kuona mabao 28 yakiwekwa wavuni katika nyasi za viwanja tofauti tofauti ulaya
Leo tutashuhudia vigogo wenzao katika mashindano haya wakipepetana na vigogo wenzao katika kusaka na kulinda heshima za klabu zao bila kusahau ule mchuano wa nani atawania kiatu cha dhahabu kama mfungaji bora wa michuano hiyo ambayo msimu uliopita iliweza kubebwa na Cristiano Ronaldo kutoka Galacticos Real Madrid.

REKODI ITAJIRUDIA TENA

Kama isemavyo "Rekodi zimewekwa ili zivunjwe" ndiyo kama tulivyoshuhudia msimu uliopita klabu ya Real Madrid iliyoweza kuiletea kwa mara ya kwanza kombe hilo lenye historia ya aina yake barani ulaya.
msimu huu pia mabingwa hawa bado wanapewa nafasi kubwa ya kuweza kufanya vizuri kutokana na ukomavu wa wachezaji katika kikosi chao pamoja na mbinu rahisi za kupata ushindi kutoka kwa kocha Zizzou.

VITA VYA UFUNGAJI

Vita vya msimu huu naweza kusema itakuwa na utofauti kwani klabu zimejipanga vizuri kwa kufanya usajili wa washambuliaji hatari na hii walau italeta tofauti na misimu  kadhaa ilyopita ambayoo ilikuwa ni vita vya mafahali wawili tu MESSI na RONALDO.

MAKOCHA NAO HAWAPO NYUMA

Lcha kuona kandanda safi likitandazwa bado tutashuhudia vita vikali baina ya makocha hodari wanaoheshimika kutokana na srekodi walizo jiwekea, watataka kudhihirisha kwamba wao bado wanamakeke tena zaidi ya awali.

HUENDA ZIKAWA FAINALI ZA MWSHO KWA  BAADHI YA WACHEZAJI

Ndiyo, kwani idadi kubwa ya wachezaji katika mashindano haya wana umri zaidi ya miaka 30 na miongoni mwa wachezaji hao ni pamoja na supastaaa wa Real madrid pamoja na mastaa wengine wakina Gianluigi, Buffon,Modric, Iniesta, Robben, Neur na wengine wengi.
Hii inaweza kutoongezaz msisimko vile vile kwani wazee hawa hawataitaji kuistaafu bila kuweka heshima zao katika michuano hii ya ulaya kwa kutumia fursa ya wakati ni muda ndugu zetu twaweza.

NAFASI KWA CHIPUKIZI KUISHANGZA DUNIA

Michuanoo hii pia naingalia kama njia pekee ya dunia kuona vipaji maridhawa vya vijana wanaochipukia katika mbio za kuvunja rekodi za magwiji wa soka Pele na wakina Gerd muller
Chipukizi ni wengi katika michuano hii na wanaonekana kufanya vizuri sana walivyokuwa katika klabu zao na hii italeta chachu zaidi kama vijana hawa wakituonesha uwezo mkubwa  zaidi ya matarajio yetu wapenda soka.

No comments:

Post a Comment

Pages