LIVERPOOL INAVOWATESA MASHABIKI WAKE - BZONE

LIVERPOOL INAVOWATESA MASHABIKI WAKE

Share This
NA TAGATO JAMES
SPORTS: Usiku wa Uefa  champions league umekamilika, huku baadhi ya vigogo wakiondoka na furaha kwa kuibuka na ushindi wa haja. timu kama ReaL madrid ya hispania Tottenham na Manchester city kutoka England zimeondoka kifua mbele katika mechi zao za kwanza za ufunguzi wa hatua ya makundi.

Tatizoo ni kule kwa majogoo wa Anfield ambao wao wamelazimishwa sare ya Nyumbani na wagumu Sevilla fc kutoka hispania ambayo kwangu imeleta maswali kadhaa ambayo nazidi kupata wakati mgumu kutafutia majibu yake.

1.Je tatizo ni liverpool au ni Ubora wa Sevilla?
  
   Huwezi kukataa kuwa katika  timu ngumu na ligi bora ya la liga Sevilla ni moja wapo kwa hivi sasa kutokana na ubora wa kikosi walio nao, mtu kama steven Nzonzi na Jesus Navas wanaifanya Sevilla kuwa pale ilipo hivi sasa ila bado haikupi wakati wagumu kuona ubora wa Liverpool kuanzia golikipa mpaka mshambuliaji wa mwisho.  kama unaweza kuwa sadio Mane halafu kwenye mbao yako una philipe countinho unataka nini kwenye dunia hii ya soka la pesa na usaliti wa kimapenzi?

Liverpool kwa kiasi kikubwa imeumiliki mchezo haswa katika eneo la katikati kuelekea mbele ya lango la wapinzani wao kuna uelewano mkubwa mno kati ya ya sadio mane, mohamed salah na Robert  firmino ambao wao kimsingi ndio wanaofanya liverpool kupata matokeo kwenye kila mchezo

2. Liverpool inakosea wapi? 

kikubwa nadhani jurgen klopp kunajambo anatudanganya hapa hasa anawaperemba wale wapenzi na wakereketa wa liverpool nalo ni ukuta wa timu yake bado hauko imara na umekuwa na nyufa nyingi mno mpenzi wa soka anaweza kuizitambua nyufa hizo. 

ukuta wa klopp haujaanza kuonyesha madudu msimu huu tu pekee baada ya kupokea kichapo cha aibu mbele ya Guardiola la hasha  bali muda sana na kwa wapenzi  wengi tuliamini  hiyo ndio itakuwa sehemu ya kwanza klop kuitazama kabla dirisha halijafungwa lakini kocha huyo alitema  huku akafukia  huku na tukaelewa yaani alituletea salah kwenye kikosi akafunga anaingiza speed kwenye safu ya ushambuliaji na akatuaminisha kuwa njia sahihi ya kuzuia na kushambulia nasi tukaamini lakini taratibu taratibu majibu anayaona.
yapo mambo mengi pia yanayoo ihukumu liverpool kama timu kutokufanya vizuri pia ikiwemo ufinyu wa kikosi pia tazama chelsea, manchester city na manchester united walivyo na vikosi vipana hiyo inawapa nafasi wachezaji kupumzika na kuwa sawa miili yao kwajili ya kila mchezo.

Liverpool imekuwa ni ya kikosi kile kile kila mechi na kitu ambacho kwa timu kitaumiza sana upatikanaji wa matokeo sio kwamba liverpool haina watu hapana bali hata walio nje wengi ni hawana uzoefu wa kutosha kuanza kupambana katika michuano mikubwa.

wakati haya yanampata klopp inabidi akumbuke sababu za kumtoa sakho katika kikosii basi azitumie hizo hizo kufanya mabadiliko mapema ili kuirudisha liverpool katika makali yake mbele tayari ipo vizuri katika ushambuliaji inabidi upande wa beki pia ajiimarishe zaidi katika dirisha dogo.

No comments:

Post a Comment

Pages