Wallice Karia amechaguliwa kuwa Rais wa TFF. - BZONE

Wallice Karia amechaguliwa kuwa Rais wa TFF.

Share This
SPORTS: Rais mpya wa TFF ametangazwa Dodoma, Matokeo ya uchaguzi mkuu wa viongozi wapya wa TFF yametangazwa rasmi mjini Dodoma baada ya zoezi zima la uchaguzi kukamilika.
Rais mpya wa TFF ni Walace Karia ambaye ameshinda kwa kura 95 kati ya 128 za wajumbe waliopiga kura kwenye uchaguzi huo. Karia amewashinda Iman MadegaShija RichardAlly MayayEmanuel Kimbena Fredrick Mwakalebela ambao walikuwa wakiwania nafasi ya urais wa TFF.
Kabla ya kuchaguliwa kuwa Rais wa TFF, Karia alikuwa makamu wa Rais chini ya Jamal Malinzi ambapo baadae aliendelea kuiongoza TFF baada ya Malinzi kuwa mahabusu akikabiliwa na mashitaka ya matumizi mabaya ya ofisi.

No comments:

Post a Comment

Pages