Rooney ambaye ndie mfungaji wa muda wote ndani ya klabu ya United baada ya kuichezea michezo 559 na kufunga mabao 253 na kurudi Everton tangu anodeke miaka 13 iliyopita amesisitiza kuwa miongoni mwa wachezaji watakao kuja nchini, kuanza mazoezi ya pamoja na wenzake, amesema kuwa atakuwemo kwenye msafara huo chini ya Kocha Ronald Koeman.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 alijiunga na Toffee alipokuwa na umri wa miaka 9 pekee ndani ya viunga hivyo vya Goodison kisha kujiunga na United mwaka 2004 na kuwasaidia kutwaa mataji ya Champions League, Europa League, mataji Nagano ya Premier League , mojo la FA Cup, matatu ya League Cups na moja la FIFA Club World Cup.
No comments:
Post a Comment