OZIL KUENDLEA KUKIPIGA ASERNAL, SANCHEZ GIROUD BADO TIA MAJI TIA MAJI - BZONE

OZIL KUENDLEA KUKIPIGA ASERNAL, SANCHEZ GIROUD BADO TIA MAJI TIA MAJI

Share This
SPORTS: Kiungo wa klabu ya soka ya Arsenal Mesut Ozil ameweka wazi nia yake ya kutaka kuendelea kubaki katika klabu ya Arsenal na atafanya mazungumzo na Klabu yake baada ya kumalizika kwa Mechi za maandalizi kwaajili ya Msimu ujao.
Kiungo huyo mwenye Miaka 28 ambaye Mkataba wake unamalizika Mwaka 20
18 amezungumza na kituo cha Klabu hiyo cha Arsenal.com na kueleleza kuwa chaguo lake ni kutaka kusalia katika timu ya Arsenal yenye Maskani yake jijini London.
“Kiukweli chaguo langu ni kuendelea kubaki Arsenal, kipindi ambacho watu wote watarejea London, tutakaa chini na Uongozi ili kujadili hatma yangu. Kama nilivyosema mwanzo kuwa ninajiskia vizuri nikiwa Arsenal. Alisema Ozil alipohojiwa na kituo cha Arsenal.com.
Ozil ambaye ni Mjerumani amekuwa akihusishwa kuondoka katika Klabu ya Arsenal huku Vilabu vikubwa Barani Ulaya ikiwemo Buyern Munich pamoja na Manchester United vikiwa vinamuwania Kiungo huyo ambaye amebakiza mwaka mmoja kwenye Mkataba wake.  Wachezaji kadhaa wa Arsenal walihojiwa na kituo hicho kabla ya kusafiri kuelekea Sydney ambako itaweka Kmabi kujiandaa na Msimu ujao, Miongoni mwa Wachezaji hao ni Pamoja na Oliver Giroud pamoja na Alexis Sanchez ambao pia wamekuwa wakihusishwa kuondoka Arsenal Kabla ya Msimu ujao kuanza. Giroud akihusishwa na klabu ya West ham United huku Sanchez akihusishwa na Manchester City pamoja na Buyern Munich.

No comments:

Post a Comment

Pages