YANGA NAYO YAGALAGAZWA NA LEOPARDS YA KENYA - BZONE

YANGA NAYO YAGALAGAZWA NA LEOPARDS YA KENYA

Share This
SPORTS: Wawakilishi pekee wa Tanzania waliobakia katika mashindano ya kombe la SportPesa Super Cup, Dar Young Africans (Yanga) imetupwa nje katika hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo. Yanga wametolewa katika kombe hilo na AFC Leopards ya Kenya kwa mikwaju ya penati 4-3.
Mchezo huo ambao ulikuwa wa vuta ni kuvute kwa pande zote mbili kulisakama lango la mpinzani wake umemalizika dakika 90 bila ya timu yoyote kuchomoza na ushindi. Sasa Leopards wanamsubiri mshindi kati ya Gor Mahia dhidi ya Nakuru katika mchezo wa fainali ambao utachezwa Jumapili hii katika uwanja wa Uhuru.

No comments:

Post a Comment

Pages