BROWN MAUZO AKIRI KUKAMATWA NA POLISI, MKASA MZIMA HUU HAPA - BZONE

BROWN MAUZO AKIRI KUKAMATWA NA POLISI, MKASA MZIMA HUU HAPA

Share This
BROWN MAUZOENTERTAIMENT: Msanii wa muziki wa zazi kipya kutoka nchini Kenya anayefanya poa na ngoma yake ya ‘Nimchague Nani’ Fredrick Mtindaa.k.a Brown Mauzo amethibitisha kukamatwa na polisi kwa makosa ambayo amebainisha kuwa hayakuhusiana na kazi yake mpya kama ilivyoripotiwa na baadhi ya mitandao nchini Kenya.
Akisawazisha uvumi huo juu ya tukio la kutiwa mbaloni sambamba na kuwekwa pingu mkononi Brown amesema kuwa ni kweli alikamatwa na polisi na kuwekwa chini ya ulinzi kwa muda kisha kuachiwa huru muda mfupi baadae baada ya kufuta taratibu za kisheria.
Awali uvumi na taarifa sisizo za kuaminika zilisema kuwa kukamatwa kwa Brown ilitokana na matumizi ya picha ya msanii ‘Akothee’ ambaye kipindi cha nyuma wawili hao walitajwa kuwa katika mahusiano ya kimapenzi.
“kushikwa nilishikwa lakini sikukaa ndani, pia ilikuwa haiambatani na nyimbo ni vitu tofauti na hiyo nyimbo lakini stori zilizotoka nje nikazisikia kwamba ni kwasababu ya wale watu baadhi ya wale walikuwa kwenye ile video lakini ilikuwa ni issue tofauti” Alisema Brown kupitia kipindi cha Udaku Sasa cha Ntv Kenya.

No comments:

Post a Comment

Pages