
Warriors wameibuka na ushindi wa vikapu 132-113 dhidi ya Cavs ukiwa ni mchezo wa 14 mfululizo kwa Warriors bila kupoteza pia ni ushindi wa pili kwa Warriors katika fainali hizi za mwaka 2017 dhidi ya Cavs.
Katika mchezo huo uliopigwa usiku wa kuamkia leo rekodi kadhaa zimevunjwa na nyingine kuwekwa ikiwemo ya LeBron James wa Cavaries kuwa mchezaji wa pili katika historia ya wachezaji wenye pasi nyingi za mwisho “assist” katika historia ya fainali za NBA huku Stephen curry na Kevin Durant wa Warriors wakiweka rekodi ya kuwa wachezaji wa kwanza kutoka timu moja kufikisha usawa wa alama zaidi ya 30 katika mechi mbili za mwanzo za fainali za NBA.
Ushindi wa Wariors usiku wa jana ulikua ni furaha kwa kocha wao Steve Kerr ambae alirejea katika timu kwa mara ya kwanza tangu Aprili 19 kutokana na kusumbuliwa na maradhi.
No comments:
Post a Comment