SIRI YA KUFANIKIWA KIMUZIKI NI KUTOBWETEKA NA KUJIONA MKUBWA – NEDY MUSIC - BZONE

SIRI YA KUFANIKIWA KIMUZIKI NI KUTOBWETEKA NA KUJIONA MKUBWA – NEDY MUSIC

Share This
ENTERTAIMENT: Nedy Music ni msanii kutoka visiwani Zanzibar ambaye kwa sasa yupo kwenye mikono ya mmiliki wa lebo ya PKP. Ommy Dimpoz.  msanii huyo mwenye sura ya upole ili kufahamu ana mchango gani kwa wasanii wenzie aliowaacha Zanzibar.
“Kwanza kabisa nafikiri kauli ambayo naweza ni kwamba kujituma zaidi na zaidi na kutokuchoka kwasababu yupo ambaye anaweza akawa anajiamini kujiona mkubwa lakini ukubwa hauwezi kukusaidia kama hautafanya vitu vikubwa,” amesema.
“Kwahiyo kwangu mimi naweza kusema kwamba tuendelee kujituma ili tuendelee kufanya vile vilivyo bora. Mchango wangu labda ni kauli tu kwasababu bado sijawa na nafasi ya kuwa na mchango wa kumsaidia mtu kwa sasa kwasababu mi mwenyewe nipo kwenye safari, nikifanikiwa zaidi basi nitasaidia,” amesema.

No comments:

Post a Comment

Pages