SALAH AVUNJA REKODI YA USAJILI NDANI YA LIVERPOOL - BZONE

SALAH AVUNJA REKODI YA USAJILI NDANI YA LIVERPOOL

Share This
SPORTS: Liverpool wamekamilisha dili la usajili winga Mohamed Salah, kutoka As Roma ya Italia, kwa dau la Pauni million 39.
Usajili wa winga huyu umevunja rekodi ya usajili kwa wachezaji waliowahi sajiliwa na timu hiyo ambapo usajili wa gharama zaidi ulikuwa wa mshambuliaji Andy Carrol, aliposajiliwa kwa dau la pauni milioni 35 mwaka 2011.
Salah raia wa Misri mwenye umri wa miaka 25 amesaini mkataba wa miaka mitano kuweza kutumikia Liverpool.
''Ninafuraha sana kuwepo hapa nitajitoa kwa asilimia mia moja na nitatoa kila kitu kwa ajili ya klabu hii, kiukweli nataka kushinda kitu nikiwa na timu hii", alisema Salah baada ya kukamilisha usajili huo.

No comments:

Post a Comment

Pages