PEREZ KUWA RAIS WA REAL MADRID MPAKA 2021 - BZONE

PEREZ KUWA RAIS WA REAL MADRID MPAKA 2021

Share This
SPORTS: Klabu ya Real Madrid itaendelea kuwa chini ya Raisi Frolentino Perez kwa kipindi cha miaka mingine minne mpaka mwaka 2021, hii ni baada ya Raisi huyo kushindwa kupata mpinzani katika uchaguzi mkuu wa klabu hiyo.
Mwisho wa kuchukua fomu kwaajili ya kugombea nafasi ya Uraisi ilikua ni siku ya Jumapili usiku, Juni 18 lakini hakuna mpinzani aliyejitokeza hivyo kumpa nafasi Perez kuendelea kuingoza klabu hiyo.
Perez,70 ameiongoza Real Madrid kwa kipindi cha miaka 17 tangu mwaka 2000 aliposhinda Uraisi akichukua nafasi ya Lorenzo Sanz aliyekua amemaliza muda wake. Katika Uongozi wake, klabu hiyo imeweka historia ya kutwaa kombe la Ulaya ‘UEFA Champions’ mara mbili mfululizo na kuwa klabu pekee kuwai kufanya hivyo katika historia ya mashindano hayo.
Lakini pia Frolentino Perez ndiye aliyeleta dhana ya Real Madrid kutumia pesa nyingi kufanya usajili wa nyota wakubwa kuanzia kwa Luis Figo mwaka 2000 akifuatiwa na nyota wengine wakubwa kama vile Zinedine Zidane mwaka 2001, Robinho bila kusahau Cristiano Ronaldo mwaka 2009 akitokea Real Madrid ambaye aliweka historia ya kuwa mchezaji ghali Duniani kwa kiasi cha Paundi Milioni 80 .
Moja kati ya vitu vinavosubiriwa na mashabiki wa Real Madrid ni tamko la Raisi huyo kuhusiana na suala la mchezaji Cristiano Ronaldo kutaka kuondoka msimu huu, pamoja na taarifa za usajili wa Kylian Mbappe kutoka AC Monaco ambaye anatajwa kuwaniwa na klabu hiyo kwa udi na uvumba.

No comments:

Post a Comment

Pages