NADAL AFANIKIWA KUTWAA TAJI LA FRENCH OPEN - BZONE

NADAL AFANIKIWA KUTWAA TAJI LA FRENCH OPEN

Share This
SPORTS: Muhispania Rafael Nadal amefanikiwa kushinda taji la michuano ya French Open baada ya kumshinda mpinzani wake Stan Wawrinka katika pambano la Fainali ya michuano hiyo iliyofikia tamati jana jijini Parisi nchini Ufaransa.
Nadal, 31 ameshinda kwa jumla ya seti 6-2 6-3 6-1 dhidi ya Mswisi Wawrinka na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Tenesi kushinda ubingwa huo mara mara kumi, ikiwa ni ‘Gland Slam’ yake ya 15 idadi kubwa zaidi kwa Mchezaji yoyote katika mchezo wa Tenesi.
Kwa sasa Nadal anashikilia nafasi ya tatu kwa ubora katika orodha ya wacheza Tenesi kwa upande wa Wanaume mbele ya Andy Murray, Novak Djokovic pamoja na Stan Wawrinka viwango ambavyo vilitolewa Mei 29 mwaka 2017

No comments:

Post a Comment

Pages