FA YAMPIGA FAINI MOYES - BZONE

FA YAMPIGA FAINI MOYES

Share This
SPORTS: Chama cha soka nchini Uingereza FA kimempiga faini David Moyes ambae alikuwa kocha wa Sunderland kwa kosa la kumtisha kumpiga kibao mwandishi wa BBC lililotokea mwezi Machi.
Moyes amepigwa faini ya Paundi 30,000 na chama hicho kufuatia tukio ambalo alilifanya tarehe 11 mwezi Machi mwaka huu kwa kumwambia mwandishi wa kike wa BBC Vicki Sparks atampiga kibao baada ya kuulizwa swali la hatima yake klabuni hapo.Tukio hilo lilitokea baada ya Sunderland kutoka sare na Burnley katika mchezo wa Ligi kuu nchini Uingereza.Photo published for David Moyes fined £30,000 after 'slap' comment to female reporter
Licha ya David Moyes kuomba msahama mapema mwezi Machi na kuonesha kujutia tukio hilo FA wamemtoza faini hiyo kutokana na lugha ya vitisho kwa mwanamke ambayo ni kinyume na taratibu na kanuni za mchezo huo.
Kwa sasa kocha huyo yupo huru baada ya kujiuzuru katika klabu ya Sunderland iliyoshuka daraja msimu huu. David Moyes amewai fundisha pia vilabu vya Everton pamoja na Sunderland kutoka nchini Uingereza.

No comments:

Post a Comment

Pages