DIAMOND ATIMIZA MAJUKUMU YAKE KWENYE ‘FATHER’S DAY’ - BZONE

DIAMOND ATIMIZA MAJUKUMU YAKE KWENYE ‘FATHER’S DAY’

Share This


MIX: Diamond Platnumz anauishi ule usemi kuwa ukipenda boga, penda na maua yake. Katika kutimiza majukumu yake kama baba kwenye Father’s Day Jumapili hii, hitmaker huyo wa Marry You, amewafanyia shopping ya kukata na nundu watoto wa kiume wa mchumba wake Zari aliyezaa na marehemu Ivan Semwanga.

Kupitia Snapchat, baba huyo wa watoto wawili, alionekana akiwa mall mjini Pretoria nchini Afrika Kusini akiwachagulia viwalo watoto wa Zari huku wao wakiwa nyuma yake. Hatua hiyo imekuja wiki kadhaa baada ya baba yao kufariki.
Kwa kitendo hicho, Diamond anaonesha kuyakubali majukumu yake kama baba wa kambo kwa watoto hao. Na kwa upendo huo, ni wazi kuwa anakuwa nao karibu zaidi kuliko zamani.

No comments:

Post a Comment

Pages