CHRIS BROWN APIGWA MARUFUKU KUMSOGELEA TRAN - BZONE

CHRIS BROWN APIGWA MARUFUKU KUMSOGELEA TRAN

Share This
ENTERTAIMENT: Mahakama imemuamuru Chris Brown kutomsogolea Karrueche Tran kwa kipindi cha miaka mitano.
Hiyo ni kutokana na Chris kumtolea vitisho mpenzi wake huyo wa zamani mwenye miaka 29.
Kwa mujibu wa TMZ, muigizaji huyo alitoa ushahidi wake mahakamani Alhamis hii. Kwenye maelezo yake, mrembo huyo alisema baada ya kuachana, Brown alimtaka airudishe pete almasi aliyomnunulia, alipokataa akawa mkali.
Alidai kumtumia message zilizosema: ‘I’m not being nice to you no more, if I see you out in public again and I’m there I will make you hate me even more, don’t be anywhere I’m out in public, I’m going to ban you from all events.’
Pia alidai ujumbe mwingine ulisema, ‘B*tch I will beat the s**t out of you’; and ‘I promise you I will make your life hell’; and ‘I can get my money back and I’m tired of playing games.”
Pia Chris aliwahi kuandika, ‘Imma kill blood’ chini ya picha ya mrembo huyo akiwa na muigizaji Michael B. Jordan. Karrueche aliimbia pia mahakama kuwa Chris aliwahi kumpiga walipokuwa pamoja.
Hata hivyo mwanasheria wa Brown, David Gammill, alisema Karruache alimdhihaki mteja wake kwa kusema aliziuza pete zake. Alimhoji pia kwanini hakuwa kuripoti tukio lolote polisi. Brown hakuwa mahakamani Alhamis hii na alikataa ombi lake la kuungana naye kwa simu.

No comments:

Post a Comment

Pages