
Kufuatia uchunguzi wa Bodi ya Ligi Kuu, ushahidi umepatikana kwa City wamevunja sheria za Ligi. Uvunjaji huo wa sheria unahusu kufanya mazungumzo na wachezaji wawili wa academy tofauti kwa ajili ya kuwasajili huku wakiwa wamesajiliwa na klabu nyingine.
Adhabu hiyo ni sawa na waliyopewa Liverpool mwezi uliopita baada ya kukutwa na hatia ya ‘kuiba’ mchezaji mwanafunzi wa shule wa Stoke City. Kuwasiliana na mchezaji wa academy yoyote akiwa amesajiliwa na klabu yake ya wakati husika ni kosa, ambalo City wamefanya na sasa linawagharimu.
No comments:
Post a Comment