HIKI NDIO KIKOSI CHA TAIFA STARS,DIDA ATEMWA KAKOLANYA NDANI - BZONE

HIKI NDIO KIKOSI CHA TAIFA STARS,DIDA ATEMWA KAKOLANYA NDANI

Share This
SPORTS: KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Salum Mayanga hajamjumuisha kipa wa Yanga, Deogratius Munishi ‘Dida’ katika kikosi cha wachezaji 23 kitakachokwenda kuweka kambi Misri kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Lesotho Juni 10, mwaka huu Uwanja wa Taifa mjini Dar es salaam.
Badala yake, Mayanga amemchukua kipa wa tatu wa Yanga, Benno Kakolanya baada ya kufanya vizuri katika mechi za mwisho za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na kuisaidia timu hiyo kutetea ubingwa.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Dar es Salaam leo, Mayanga alisema kwamba wachezaji hao wataingia kambini wiki ijayo mara baada ya mechi za mwisho za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara wikiendi hii.


Alisema mazoezi yataanza Mei 24 hadi 29 mjini Dar es Salaam kabla ya Mei 30 timu kwenda Misri kuweka kambi ya wiki moja na kurudi nchini Juni 7 kwa ajili ya mechi dhidi ya Lesotho.
Kikosi kamili cha Stars ni; Makipa; Aishi Manula (Azam), Benno Kakolanya (Yanga), Said Mohammed (Mtibwa Sugar).
Mabeki; Shomari Kapombe, Hassan Kessy, Mwinyi Mngwali, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Salim Abdallah, Aggrey Morris (Azam), Abdi Banda (Simba) na Erasto Nyoni (Azam).  
Viungo; Himid Mao (Azam), Jonas Mkude (Simba), Salum Abubakar ‘Sure Boy’ (Azam), Said Ndemla (Simba), Muzamil Yassin (Simba), Simon Msuva (Yanga), Farid Mussa (DC Tenerife, Hispania) na Shiza Kichuya (Simba).
Washambuliaji ni Thomas Ulimwengu (FC Eskilstuna, Denmark), Mbwana Samatta (KRC Genk, Ubelgiji), Mbaraka Yussuf (Kagera Sugar), Ibrahim Hajib (Simba) na Abdulrahman Mussa (Ruvu Shooting).
Ikumbukwe Mayanga anasaidiwa na Fulgence Novatus, kocha wa makipa, Patrick Mwangata, Meneja Dani Msangi, Madaktari Gilberti Kigadiya na Richard Yomba pamoja na mtunza vifaa Ally Ruvu.

No comments:

Post a Comment

Pages