BADO NASHOOT VIDEO NJE KWASABABU NATAFUTA UBORA - BZONE

BADO NASHOOT VIDEO NJE KWASABABU NATAFUTA UBORA

Share This
ENTERTAIMENT: Pamoja na kuwa sekta ya production inazidi kukua siku hadi siku hapa Bongo, kutokana na madirector wa hapa kujiongeza na kufanya vitu vikali siku hadi siku na hata kupelekea video za hapa kuchezwa kwenye vituo vyote vikubwa Afrika, bado imani ya Joh Makini haijawa rafiki kwa madirector wa hapa nchini kiasi cha kuwaamini na kufanya nao kazi.
Mkali huyo wa muziki kutoka kaskazini amedai kuwa kitu pekee ambacho kinamfanya asafiri na kwenda kufanya kazi na madirector wa nje ni ubora, Joh amedai ubora ambao anaupata akiwa nje, hana imani kama ataupata kwa madirector wa ndani japo kuwa wanazidi kukua siku hadi siku.
“Siwezi kuficha kwamba natafuta ubora, na standard ambayo nimeset katika muziki wa Joh Makini inanilazimisha kuendelea kwenda juu na sio kurudi chini, nawaamini madirector wa ndani ila kusema ukweli nakuwa comfortable nikifanya kazi na madirector wa nje kwasababu nakuwa sina stress nakuwa napata kitu ambacho nimeset na wao wanakuwa wanafanya kitu ambacho very professional”Alisema Joh Makini.
Pia Joh Makini aliongeza kuwa “Sina maana kuwa wa nyumbani sio professional, ila nafkiri wenyewe wanaelewa kuwa wanatakiwa wajipange zaidi ili waweze kwenda sambamba na ukubwa wa wasanii wao wa nyumbani ambao wako kwenye international level, lakini so far wanafanya kazi nzuri.”

No comments:

Post a Comment

Pages