JE NAMBA YAKO YA SIRI KATIKA SIMU NI YA SIRI? - BZONE

JE NAMBA YAKO YA SIRI KATIKA SIMU NI YA SIRI?

Share This
Simu ya rununuLIFESTYLE: Je wajua mtindo wako wa kushika simu unawaonyesha wadukuzi nambari yako ya siri? Jinsi unavyoishika simu yako unapoitumia inaweza kuwapa wadukuzi nafasi ya kuiba nambari yako ya siri au 'pin number', kulingana na utafiti uliofanywa.
Wataalam katika chuo kikuu cha Newcastle walichambua jinsi watu walivyozishika simu zao wakati walikuwa wakiweka nambari zao za siri na wanasema waliweza kutambua kwa usahihi wa asilimia 70 nambari zote za siri zenye tarakimu nne baada ya kujaribu mara moja tu na kwa asilimia 100 baada ya kujaribu mara tano.
Wataalam hao wa maswala ya teknolojia wanasema makampuni ya teknolojia yanayofahamu tatizo hili lakini hawajui watafanya nini.
Dkt. Maryam Mehrnezhad kutoka shule ya kompyuta sayansi ya chuo hicho amesema: "Simu nyingi aina ya 'smartphones' na 'tablets' zimewekwa sensa.Hakuna kampuni ya teknolojia iliyopata suluhu ya tatizo la programu zinazoiba data muhimu
Lakini kwa kuwa tovuti nyingi na programu za simu haziulizi ruhusa kabla ya kutumia propgramu hizi, ni rahisi sana kwa programu mbaya kupata data."
Dkt Mehrnezhad anasema kuwa: "Ukifungua kurasa kwenye baadhi ya tovuti ambazo zina programu hizo mbaya ukitumia simu yako, kisha ufungue tovuti nyingine, ile ya kwanza ina uwezo wa kunakili maelezo yote ya kibinafsi unayotoa.
"Na jambo baya zaidi ni kuwa usipofunga kurasa hizo, programu hizo zinaweza kupeleleza hata simu iwapo simu imewekwa nambari ya siri.
Watu wanashughulika sana na kamera na programu inayoonyesha ramani, GPS kuliko sensa hizo.
Wataalamu hao wamegundua kwamba kila unachofanya katika simu iwe ni kupiga simu, kuandika ujumbe au kutafuta kitu hupelekea mtu kuishika simu kwa njia fulani ya kipekee.
Kwa hivyo kwenye tovuti inayofahamika, waliweza kujua mtu amefungua ukurasa upi na nini alichokuwa akiandika, kulingana na jinsi alivyoishika simu.
Wanasema wameelezea kampuni zote kuu za teknolojia kama Google na Apple kuhusu hatari hii lakini hakuna aliyeweza kutoa suluhu hadi sasa.

No comments:

Post a Comment

Pages