Miezi michache iliyopita Baraka Da Prince alitangaza kutaka kumsaini Lord Eyez huku uongozi wa Weusi ukidai hauna taarifa hizo na wao wanazisikia tetesi hizo kupitia mitandao ya kijamii.
Akizungumzia suala hilo katika 255 ya XXL ya Clouds FM, rapper Nay wa Mitego amedai kati ya Barakah na Lord Eyez haoni wa kumuongoza mwenzake.
“Hiyo ni safari ya kipofu na kiziwi, naweza kusema hivyo. Kiukweli haimake sense, kwasababu mtu ambaye anataka kuongozwa na yeye akamuongoza mwenziye ndio maana ya mfano wangu. Kibaya zaidi Lord Eyez ni mkubwa zaidi ya Baraka. Sawa kuna watu ambao wanasimamiwa na watu wadogo lakini ukiangalia pale alipo msanii kama Baraka anahitaji msaada zaidi.”
Suala hilo limeleta mjadala katika mitandao ya kijamii huku wengi wakiendelea kusubiri kuoa itakuwaje.

No comments:
Post a Comment