SPORTS: Mshambuliaji wa klabu ya Barcelona, Luis Suarez amedai kuwa ana matumaini ya kwamba rufani yake itakayokatwa itaweza kumuokoa asikose mchezo wa fainali ya Copa del Rey baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu katika mchezo wa nusu fainali ya mkondo wa pili dhi
di ya Atletico Madrid.
Suarez aliifungia Barcelona bao katika mchezo ambao ulishuhudia wachezaji watatu wakipewa kadi nyekundu katika sare ya bao 1-1 jana iliyofanya Barcelona kufuzu fainali ya nne mfululizo kwa jumla ya mabao 3-2.
Hata hivyo nyota huyo wa kimataifa wa Argentina alitolewa nje kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka mitatu aliyokaa Barcelona baada ya mwamuzi kudhani alimpiga kiwiko Koke katika dakika za majeruhi.
Katika mahojiano na Gol TV, Suarez amesema kadi hiyo aliyopewa inamfanya ajisikie kucheka kwani inaonekana kama mwamuzi alidhamiria kufanya hivyo. Suarez aliendelea kudai kuwa wanataka kuona kama wanaweza kukata rufani kwasababu hadhani kama alifanya kosa lolote kustahili adhabu hiyo.
No comments:
Post a Comment