DJ KHALED MATATANI KWA KUIBA MDUNDO WA ‘I GOT THE KEYZ’ - BZONE

DJ KHALED MATATANI KWA KUIBA MDUNDO WA ‘I GOT THE KEYZ’

Share This
ENTERTAIMENT: Tukiwa tunasheherekea ujio mwingine wa album mpya Dj Khaled “Grateful”, ishu kubwa nyingine imeibuka kwamba Dj Khaled anashitakiwa kwa kuiba beat la “I got The Keyz”.
Kupitia ripoti ambayo imetolewa na producer Chris Hill anaye dai kwamba mdundo wa ngoma ya“I got the Keys” ambao Dj Khaled aliwashirikisha Jay z pamoja na Future, amefunguka kusema mdundo huo ni wake na aliutengeneza na kuwahi kumpatia Dj Khaled kipindi hicho cha mwaka 2008.
Chris Hill aliendelea kufunguka kwa kusema kwamba alikutana na Dj Khaled ndani ya klabu hukoAtlanta mwezi October katika mwaka huo wa 2008 na kumpatia Dj Khaled CD ya mdundo huo ambao Khaled akuwahi kuongea chochote mpaka alipousikia ule wimbo kupigwa ukiwa na mdundo wake kutoka kwenye album ya “Major Keyz’.
Dj Khaled hayupo peke yake ambaye anashitakiwa na producer huyo, Hills amewashitaki hadiSony Music pamoja na maproducer wengine waliousika kwenye ngoma hiyo ya “I got The Keyz”ambayo imewaingizia mkwanja mwingi.

No comments:

Post a Comment

Pages