Rapper huyo ambaye pia ni member wa Tamaduni Music, ameadai video ya wimbo huo imekuwa ni video yake ya kwanza kuwa na views wengi kwa muda mchache.
“Kwa muda mfupi toka video itoke imeonyesha utofauti mkubwa sana katika muziki wangu, ni video yangu ya kwanza imeangaliwa zaidi YouTube kwa muda mchache. Pia ni wimbo ambao umeleta impact kubwa sana kwenye muziki wangu,” Songa aliiambia Planet Bongo ya EATV.
Katika hatua nyingine rapper huyo amedai kuna watu wengine wanamwambia kwamba amebadilika.
“Watu sasa hivi wanasubiri ngoma mpya ili kuona kama ndo nimebadilika kabisa au nimegusa tu huku,” alisema Songa.
No comments:
Post a Comment