SAMBA INAMIUJIZA YAKE,Garrincha alikuwa ni Genius wa mpira lakini Starehe ikampoteza. - BZONE

SAMBA INAMIUJIZA YAKE,Garrincha alikuwa ni Genius wa mpira lakini Starehe ikampoteza.

Share This
 Pele once said, "Garrincha could do things with the ball that no other player could"Alizaliwa  kwenye kijiji cha Pau Grande kwenye mji wa Rio De Janiero tarehe 23 Oktoba mwaka 1933, jina lake kamili ni Manuel Francisco Dos Santos almaarufu kama 'GARRINCHA'.




Kutoka kwa sister Rosa alipewa jina la 'Wren' likiwa na maana ya fundi wa mguu linaweza likawa jina gumu sana kwako lakini ilo ndo jina ambalo lingemfaa kutokana na ufundi wa mpira aliokuwa nao ata asipofanya mazoezi.



Akiwa kwenye Career yake ya soka akiwa anakaribia miaka 20 alitumia mda wake Botafogo, alikuwa na mng'aoo pekee Duniani akiwa na uwezo binafsi wa kuumiliki mpira na watu wengi wakiwa wanatumia maneno haya ya kingereza kwake yeye 'God Giving Gift for Dribbling'



Aliweza kunyakua makombe mawili ya kombe la Dunia akiwa na Brazil akichukua mpira wa dhahabu na kiatu cha dhahabu nchini Sweden mwaka 1962.

Lakini kwakile alichozawadiwa uwanjani alikuwa anakifanyia mzaa.

Kwasababu alikuwa baba pale alipokuwa na miaka 20 na akiwa babu pale alipofikia miaka 40 na maisha yake alipata nayotabu pale alipokuwa anatumia vilevi.
 Pele once said, "Garrincha could do things with the ball that no other player could"
Lakini Pale alipokuwa anacheza mpira ulikuwa umewekwa gundi kwenye mguu wake alikuwa mtu wa ajabu sana moja ya kipaji ambacho akijawahi kuonekana Duniani.

Alipoanza maisha yake alipata tabu sana kwasababu mguu wake wa kulia ulikuwa mfupi sana kushinda wa kushoto na kikamfanya ata Garrincha kuweza kutumia mguu wa kushoto.

Alipoanza kujitambulisha kwenye soka mapema tuu akapata jina jipya la utani toka kwa mashabiki wa soka "O Anjo de pernas Tortas" ikiwa na maana ya 'Malaika alekuwa na miguu iliokunjika'

 After leaving his first wife Nair Marques, Garrincha soon began dating singer Elza Soares, right

Garrincha ilivofikia mwaka 1952 aliweza kupata mke wake wa kwanza ambae alijulikana kama Nair Marques ambae alipata nae watoto nane wa kike lakini baada ya mda kidogo akamuacha na kwenda kwa mwanamke maarufu wa Kibrazil ambae alikuwa mwanamziki alikuwa akijulikana kama Elza Soares.

Vile vile mkali huyu alikuja fanikiwa kupata watoto 14 na wanawake watano tofauti kiukweli ni ya kushtukiza sana kwasababu kiukweli alipataje mda wa soka uwanjani.

 After he retired, Garrincha turned to the bottle, sometimes drinking a bottle of rum a day

Usinisikilize mimi na maneno yangu hebu msikilize Pele mchezaji pekee alieweza kushinda makombe matatu ya Dunia. kati ya mwaka 1957 na 1962 ni rahisi sana alikuwa ashikiki alifika kwenye fainali za kombe la Dunia mwaka 1962 Zenith na kujikuta ni mfungaji bora mwishoni mwa shindano ilo Garricha ndio alievunjaga matumaini ya Uingereza mwaka huo pale alipokatisha ndoto za Uingereza kwa kuwachapa mabao 3-1.

 Garrincha may be gone but he'll never be forgotten

Garrincha mchezo wake wa 50 ndio ulikuwa mchezo wa mwisho kwenye taifa lake la Brazil dhidi ya Hungary kwenye dimba la Goodison park kwenye fainali za kombe la Dunia mwaka wa 1966. Katika mchezo huo Brazil walipoteza kwa magoli 3-1 na baada ya ushindi mara 43 na kupata sare sita na ndio ilikuwa kwa mara ya kwanza wanaonekana kushindikana akiwa amevalia Jezi ya taifa.

 Garrincha's booze battles were said to have been heightened after he killed his mother-in-law

Kama baba yake ambae alikufa kwa matumizi ya pombe kupitiliza alijikuta na yeye akiingia kwenye dimbwi ilo ilo la Ulevi pale alipoacha kucheza soka na kujikuta akiwa na pombe mda wote, Garricha alikufa Januari 20 1983 kutokana na Ugonjwa wa Cirrhosis akiwa na umri wa miaka 49.

No comments:

Post a Comment

Pages