SPORTS:
Inaonekana kuwa siku njema kwa Antonio Conte na ameamua kutumia washambuliaji wake wote wawili. Wote wameshinda na kusongesha timu, Olivier Giroud alifunga goli la kwanza lenye juhudi kubwa sana kabla ya kipindi cha kwanza na baada ya kipindi cha kwanza kwenye kipindi cha pili kwenye dakika ya 86 Alvaro Morata alliipa Chelsea goli la pili na la ushindi.
Kulikuwa na nafasi kadhaa kwa Southampton pia walikuwa hatari sana kwenye eneo la wanadarajani hasa pale kocha Mark Hughes alipompeleka Nethan Redmond na Dusan Tadic kwenye eneo la ushambuliaji tunaweza tukasema kuwa Caballero alikuwa mwokozi mzuri wa Chelsea na ndo alitakiwa kuwa nyota wa mchezo.
Sasa Chelsea watarudi tena kwenye dimba la Wembley kucheza na vijana wa Jose Mourinho kutokea kwenye klabu ya Manchester united ambao jana waliibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Tottenham Hotspurs fainali itaenda kupigwa tarehe 19 Mei 2018.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Bwherever is a Tanzanian Radio Personality and Blogger who initiative Bbaseonpoint blog.
No comments:
Post a Comment