WEST HAM UNITED KARIBUNI KUMNYAKUA CHACHARITO - BZONE

WEST HAM UNITED KARIBUNI KUMNYAKUA CHACHARITO

Share This
SPORTS: West Ham wanakaribia kufanikiwa kumnunua mshambuliaji wa Mexico Javier Hernandez kutoka kwa klabu ya Bayer Leverkusen ya Ujerumani.
Klabu hiyo ina matumaini makubwa ya kufanikiwa kumchukua mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United, 29, ingawa kufikia sasa hawajakamilisha makubaliano kuhusu bei yake.
Hayo yakijiri, mshambuliaji wa Austria Marko Arnautovic anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu katika klabu hiyo katika saa 48 zijazo baada ya West Ham kuafikiana na Stoke City.
West Ham walikuwa wamewasilisha dau mara mbili zikikataliwa lakini sasa inaarifiwa Stoke wamekubali dau la karibu £24m.
Mwezi Mei Hernandez - ambaye hujulikana sana kwa jina la utani la Chicarito, aliibuka kuwa mfungaji bora zaidi wa Mexico katika historia baada ya kufunga bao lake la 47. Hernandez alifunga mabao 59 katika mechi 156 alizochezea United tangu alipotua Old Trafford mwaka 2010, kabla ya kuhamia Leverkusen kwa£7.3m mwezi Agosti 2015.
Amefungia klabu hiyo ya Ujerumani mabao 39 katika mechi 76.

No comments:

Post a Comment

Pages