CHEKI JINSI JAMES HARDEN ALIVOWAPIKU STEPH CURRY, RUSSELL WESTBROOK - BZONE

CHEKI JINSI JAMES HARDEN ALIVOWAPIKU STEPH CURRY, RUSSELL WESTBROOK

Share This
SPORTS: Mchezaji wa timu ya Kikapu ya Huston Rockets James Harden amekubali kuongeza mkataba wa miaka minne katika timu hiyo wenye Thamani ya Dola za Kimarekani Milioni 170 ambao ni Mkataba ghali zaidi katika Historia ya NBA.
Harden ambaye alikua ni Mchezaji wa pili nyuma ya Russell Westbrook katika Kinyang’anyiro cha tuzo ya MVP (Most Valuable Player) Msimu uliopita alibakiza Mkataba wa Miaka miwili ambao ulikua na thamani ya Dola za Kimarekani Milioni 59 na baada ya kuongeza Miaka minne umefikia kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 170 na kumfanya Mchezaji huyo awe na thamani ya Dola za Kimarekani Milioni 228 kwa Mpaka Msimu wa mwaka 2022-2023.   Tangu James Harden ajiunge na Huston Rockets Mwaka 2012 akitokea katika timu ya Oklahoma City Thunder ameiongoza Huston Rocket kucheza Michezo ya Mtoano Misimu mitano huku akitangazwa katika Kikosi cha kwanza cha NBA Mara tatu ndani ya Misimu minne huku akimaliza nafasi ya Pili kwa Kura katika Kinyang’anyiro cha MVP Mwaka 2014/2015 pamoja na 2016/2017.
Pia Harden alikua ndiye Mchezaji wa kwanza katika Historia ya NBA kufunga alama 200 assist 900 pamoja na rebound 600 ndani ya Msimu mmoja.

No comments:

Post a Comment

Pages