WARRIORS WAKICHAFUA JANA KWENYE FAINAL ZA NBA - BZONE

WARRIORS WAKICHAFUA JANA KWENYE FAINAL ZA NBA

Share This
SPORTS: Timu ya mpira wa kikapu kutokea ukanda wa Magharibi Golden State Warriors wamefanikiwa kushinda mchezo wa kwanza wa Fainali ya ligi kuu nchini marekani NBA dhidi ya Cleverland Cavaries kutoka mashariki katika mfululizo wa michezo ya fainali hizo iliyoanza kupigwa usiku wa kuamkia leo Juni 2.
Warriors wameshinda kwa jumla ya vikapu 113 dhidi ya vikapu 91 huku Kevin Durant wa Warriors akiongoza kwa kutupia vikapu na kukusanya jumla ya alama 38 huku akitoa pasi za mwisho yaani ‘assist’ 10.
Baada ya ushindi huo Warriors wanafikisha jumla ya michezo 6 bila kupoteza tangu kuanza kwa mfululizo wa michezo ya nusu fainali ya ukanda wa Magharibi huku ukiwa ni mchezo wa 13 mfululizo bila kupoteza.
Cavs na Warriors wamekutana mara tatu mfululizo katika fainali hizi, huku kila timu ikipata ushindi mchezo mmoja, warriors wakishinda mwaka juzi msimu wa mwaka 2015 na Cavs msimu wa mwaka jana 2016. Warriors tayari wameanza vizuri fainali hizi za mwaka huu kwa kupata ushindi katika mchezo wa kwanza. Timu hizo zitakutana tena siku ya Jumapili katika fainali ya pili.

No comments:

Post a Comment

Pages