STEREO NDANI YA WCB....... - BZONE

STEREO NDANI YA WCB.......

Share This


ENTERTAIMENT: Rapa na hitmaker wa ngoma ya ‘Nitabaki juu’ Stereo baada ya kupokea sifa ya kukubaliwa na Staa wa muziki wa Bongo Fleva Diamond Platnumz hatua zaidi za kikazi zimebuka.

Akipiga stori na XXL ya Clouds Fm katika ujio wa ngoma yake mpya ya ‘Mpe habari’ aliyomshirikisha Rich Mavoko, Stereo amesema kuwa Diamond Platnumz amemfichulia mengi kuhusu anachokiona katika uwezo wake kimuziki hata kupewa nafasi ya kufanya kazi na WCB kwa ujumla.
“haya mambo yalianza hapa siku wakati Abwene anatambulisha Zigo Remix na Diamond, for the first time watu wakamsikia Diamond anazungumza kwamba Stereo ni moja ya rapa ambao anatamani kufanya nao kazi” Alisema Stereo.
Baada ya hilo na Diamond kumbubali Stereo, Stereo hakusita kufika ofisi za WCB kutoa shukrani zake juu ya utambuzi wa uwezo wake ambapo picha liliendelea walipofanya mazungumzo kama Stereo anavyoendelea kufunguka.
“(Diamond) akaniambia nataka ufanye kazi nataka ufanye kazi…nataka kusikia unarecord, kisingizio sio studio sio chochote…studio hiyo hapo Lizer huyo hapo na mimi nita monitor mambo yote” Aliongeza.
Rapa Stereo akisimulia hofu yake ya kufanya vitu katika muziki ambavyo havina ukubwa kulingana na ukubwa wake ameondolewa hofu hiyo na Diamond Platnumz ambapo safari ya usimamizi wa kazi zake chini ya WCB umeanza rasmi kwa kazi hii mpya aliyomshirikisha Rich Mavoko.

No comments:

Post a Comment

Pages