"MZIKI KWA SASA BONGO UMEKUA ZAIDI"; MR BLUE - BZONE

"MZIKI KWA SASA BONGO UMEKUA ZAIDI"; MR BLUE

Share This
ENTERTAIMENT: Watu wengi wanasema muziki kwa sasa umebadilika, ni wachache tu ambao bado wanaamini muziki wa Bongo upo pale pale.  Mr Blue, msanii wa kitambo ambaye mpaka sasa bado ameishikilia minyororo ya muziki tena kiumakini zaidi ili kupata maoni yake.
Amesema, “Kwa upande wangu naona muziki umekuwa sana, yaani umebadilika. Wasanii kwa sasa wanafanya vizuri sana ukilinganisha na zamani wakati tunaanza. Sasa hivi kidogo watu wamebadilika japo kuwa pia nina wasiwasi kwamba unaweza ukapotea kwasababu wasanii wamekuwa wakienda na wakati. Kwahiyo wanakuwa wanakimbia kwenye ule uasilia wa muziki.”
Ameendelea, “Lakini bado hatujapotea sana kwasababu hata ukiangalia Marekani nao pia wamepotea kwenye ule muziki wao hasa wa hiphop ladha ile watu wanayoitaka haipo tena, imekuwa ni biashara lakini si kitu kibaya.”
Aidha aliongeza kuwa yeye sio mwana hip hop, sio mtu R&B na wala sio Mbongo Flava bali mwanamuziki kwahiyo anaweza kuimba chochote.

No comments:

Post a Comment

Pages