MAYWEATHER KUZICHAPA TENA NA MCGREGOR - BZONE

MAYWEATHER KUZICHAPA TENA NA MCGREGOR

Share This
SPORTS:Bondia Floyd Mayweather atapigana na bingwa wa UFC, Conor McGregor katika pambano la uzito wa kati lililopangwa kufanyika Agosti 26 mwaka huu mjini  Las Vegas nchini Marekani.
Mayweather, 40 amethibitisha pambalo hilo kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii ya Twitter akithibitisha kuwepo kwa pambano hilo huku mpinzani wake ambae ni McGregor, 28 akiandika “The fight is on” ikiwa na maana pambalo lipo tayari. Mayweather anarejea tena ulingoni kupigana na Conor McGregor tangu alipotangaza kustaafu mchezo huo kwa mara ya pili baada ya kushinda pambano lake dhidi ya Manny Pacquiao mwaka 2015. Katika mapambano 49 aliyocheza Mayweather hajapoteza pambano lolote huku McGregor akipoteza mapambano 3 kati ya 24 aliyocheza.

No comments:

Post a Comment

Pages