LEBRON JAMES AVUNJA REKODI NBA - BZONE

LEBRON JAMES AVUNJA REKODI NBA

Share This


SPORTS: Baada ya kuipita rekodi ya mkongwe Michael Jordan ya kuwa mfungaji wa muda wote katika hatua ya mtoano mwezi uliopita, LeBron James amekuwa mchezaji wa tatu katika orodha ya wafungaji bora wa muda wote katika hatua ya Fainali za NBA zilizoendelea hapo jana.

Nyota huyo wa Cleveland Cavaliers amempita Michael Jordan kwa kufikisha jumla ya alama 1,176 baada ya kutupia kikapu cha kwanza katika mchezo wa fainali ya jana dhidi ya Golden State Warriors katika mchezo wake wa 44 wa fainali wakati Michael Jordan ambaye anashikilia nafasi ya nne alifikisha alama hizo katika mchezo wa 35.
Katika orodha hiyo King James amepitwa na wachezaji wawili ambao ni Jerry West aliyekuwa mchezaji wa Los Angeles Lakers mwenye alama 1,679 pamoja na Kareem Abdul-Jabbar ambaye aliwai kuchezea timu ya Milwaukee Bucks pamoja na Los Angeles Lakers mwenye jumla ya alama 1,317 .
Pia James ameweka rekodi nyingine katika mchezo wa jana ambao waliibuka na ushindi ukiwa ni mchezo wa kwanza kushinda katika fainali nne walizocheza. Rekodi hizo ni pamoja na kuwa mchezaji mwenye ‘Triple double’ nyingi zaidi,9 akimpita mkongwe Magic Johnson pia ameipita rekodi ya Michael Jordan ya kuwa nyota mwenye idadi nyingi ya mipira ya kurusha mbali yaani ‘Free throws’ kwa kufikisha jumla ya idadi 1,463.
LeBron James ameisaidia Cavaliers kushinda mchezo wa jana wa fainali ya nne dhidi ya Warriors katika dimba la Quicken Loans Arena kwa vikapu 137 kwa 116, mchezo wa tano katika fainali hizo utapigwa Juni 12 katika dimba la Oracle Arena.



No comments:

Post a Comment

Pages