JE UNAMJUA MWANAUME ANAYEMTAKA MALAIKA - BZONE

JE UNAMJUA MWANAUME ANAYEMTAKA MALAIKA

Share This
ENTERTAIMENT: Linapokuja suala la mapenzi au mahusiano kila mtu ana vigezo vyake kwa mwanaume/ mwanamke anayemhitaji. Muimbaji wa Bongo Flava, Malaika ametoa sifa za mwanaume anayemhitaji kwenye maisha yake ya kimapenzi.
malaika6tz-20161012-0002“Mimi katika maisha yangu ya mahusiano napenda mwanaume mwenye kujielewa. Najua ni wachache sana wapo, Pia napenda mwanaume mwenye uchambuzi wa vitu, mchapa kazi sio wa kukaa kaa tu hata kama sio kazi ya ofisi lakini awe hivyo ili tusaidiane kwenye maisha.Lakini na upendo ni kitu ambacho nakihitaji sana awe nacho mpenzi wangu na mwenye kujiheshimu ajue kwamba yeye ni mpenzi wa mtu kwahiyo awe na mipaka kwenye vitu fulani so huyo ndo mwanaume ninayehitaji kuwa naye,” ameongeza.
Ni hivi karibuni tu Malaika alirejea kutoka kwenye ziara ndefu ya Marekani.

No comments:

Post a Comment

Pages