JASON DERULO NDANI YA COKE STUDIO MSIMU HUU - BZONE

JASON DERULO NDANI YA COKE STUDIO MSIMU HUU

Share This
ENTERTAIMENT: Staa wa muziki wa RnB kutoka nchini Marekani, Jason Desrouleaux a.k.a ‘Jason Derulo’ imethibitika kuwa atadondoka nchini Kenya wiki hii kwa lengo la kupamba zaidi muendelezo na uzinduzi wa Coke studio Africa msimu mpya katika awamu hii ya tano.
Baada ya msimu wa nne ambapo alidondoshwa Trey Songz na sasa waandaaji wamebainisha kuwa ni Derulo ambaye kwasasa anatikisa na wimbo wake wa ‘Swalla’, ambapo ndani ya jumba la Coke studio atapata kushirki katika utayarishaji na wakali wawili mmoja kutoka Nigeria, Masterkraft na DJ Maphorisa wa Afrika Kusini.
Ni msimu ambao umeungansisha wasanii wa nchi zaidi ya 30 za Afrika ambazo ni Kenya, Afrika Kusini, Uganda, Tanzania, Rwanda, Ethiopia, Nigeria, Ghana, Angola, Zimbabwe, Togo, Ivory Coast, Madagascar, Mauritius, DRC, Cameroon na Msumbiji.
Hata hivyo Jason Derulo katika msimu huu ameingia katika kipengele kwenye kipindi maalum cha ‘Global Fusion Edition’!

No comments:

Post a Comment

Pages