TAIFA STARS YAANZA KUJIFUA LEO MISRI - BZONE

TAIFA STARS YAANZA KUJIFUA LEO MISRI

Share This
SPORTS: Timu ya mpira wa miguu ya Tanzania inatarajiwa kuanza mazoezi yake usiku huu baada ya kufika salama mjini Alexandria,nchi Misri kwa ajili ya kuweka kambi.
Akizungumza mara baada ya kukagua viwanja vya mazoezi leo asubuhi, Kocha Mayanga ambaye alipewa majukumu ya kuifundisha timu hiyo mapema - Januari, mwaka huu, amesema: "Programu ya mazoezi kwa timu hii itaanza leo saa 2.00 usiku. Ingawa siku nyingine nitafanya asubuhi na jioni."
Taifa Stars inayopiga kambi hapa Misri, inajiandaa na mchezo dhidi ya Lesotho utakaofanyika Juni 10, 2017 kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Mchezo huo umepangwa kuanza saa 2.00 usiku.
Mchezo dhidi ya Lesotho ni muhimu kwa Tanzania ikiwa ni mechi ya kwanza kwa Taifa Stars katika Kundi 'L' kuwania nafasi muhimu ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika NCHINI Cameroon.
Mbali ya Lesotho na Tanzania, mataifa mengine katika Kundi 'L' ni Uganda na Cape Verde ambao pia wikiendi ya Juni 9, 10 na 11, mwaka huu watakuwa katika mchezo wa kwanza pia kuwania nafasi hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages