SIMBA NA YANGA KUGOMBANIA MAMILIONI YA SPORTPESA SUPER CUP - BZONE

SIMBA NA YANGA KUGOMBANIA MAMILIONI YA SPORTPESA SUPER CUP

Share This
Image result for sportpesa in TanzaniaSPORTS: KAMPUNI ya SportPesa imeandaa mashindano maalumu ya soka yatakayo julikana kama SportPesa Super Cup  mashindano hayo yata  shirikisha timu za Tanzania, Zanzibar na Kenya. Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa Kampuni ya SportPesa Tanzania, Tarimba Abbas amesema leo katika mkutano na Waandishi wa Habari kwamba, Bingwa wa michuano hiyo atapata dola za Kimarekani 30,000 na nafasi ya kucheza dhidi ya timu ya England.
Amezitaja timu hizo kuwa Simba SC, Yanga SC na Singida United kwa Tanzania BaraJang’ombe Boys yaZanzibar, Gor Mahia, AFC Leopards, Nakuru All Stars na Tusker FC za Kenya. 
Tarimba amesema kwamba michuano hiyo itaanza Juni 5, mwaka huu hadi Juni 11 na itafanyika Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
“Tunatarajia mashindano haya yatakuwa changamoto nzuri kwa timu zote zitakazoshiriki na pia burudani nzuri kwa wapenzi wa mpira wa miguu nchini, hususan mashabiki wa timu zenyewe,”amesema Tarimba.

No comments:

Post a Comment

Pages