Ulikuwa mchezo mkali kama ilivyotarajiwa na Mali ndiyo walioutawala zaidi na pengine kutokana na serengeti boys kucheza kwa tahadhari ya kujihami zaidi.
Mali walimiliki mpira kwa muda mrefu na kupanga vyema mashambulizi yao, lakini safu ya ulinzi ya Tanzania ilicheza vizuri na kuokoa hatari nyingi ukiacha chache ambazo mabingwa hao watetezi walipoteza wenyewe. Lakini sifa zaidi zimuendee kipa wa Tanzania, Ramadhani Kabwili aliyeokoa michomo mingi ya hatari ya washambuliaji mafundi wa Gabon.
Kwa kutumia mfumo wa kushambulia kwa kushitukiza, Serengeti Boys nayo ililikaribia mara kadhaa lango la Mali, lakini wakashindwa kutumia nafasi.
Na zaidi Serengeti Boys ilipata nafasi za kufunga kipindi cha pili, huku nafasi nzuri zaidi akiipoteza Assad Ally ambaye akiwa amebaki na kipa wa Mali, Alkalifa Koulibaly kwenye akapiga ovyo mpira ukapotea.
No comments:
Post a Comment