SERENGETI BOYS KUTUPA KARATA YAO YA KWANZA LEO HUKO GABON - BZONE

SERENGETI BOYS KUTUPA KARATA YAO YA KWANZA LEO HUKO GABON

Share This
SPORTS: Timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa Miaka 17, Serengeti Boys, leo Jumatatu  inafungua pazia lake katika mashindano ya Kombe la Afrika kwa Vijana, kwa kumenyana na Mali katika michuano hiyo inayofanyika nchini Gabon.

Serengeti Boys ipo Kundi B, pamoja na timu nyingine za Angola na Niger ambazo nazo zitakuwa kibaruani leo.

Akizungumza  kwa njia ya simu jana, kocha mkuu wa kikosi hicho, Bakari Shime, alisema kuwa kikosi chake kipo vizuri na kimejiandaa vya kutosha kuwakabili vijana wa Mali kwenye mchezo huo wa kwanza.


 “Kikosi kipo vizuri na tumejipanga kuikabili vilivyo timu ya Mali kwani tunataka kuwafurahisha Watanzania kwa kutowaangusha na naomba wazidi kutuombea,” alisema Bakari Shime.

No comments:

Post a Comment

Pages